HabariMilele FmSwahili

Waziri Chelugui : Kaunti ya Nairobi kuendelea kushuhudia uhaba wa maji kwa muda

Kaunti ya Nairobi itaendelea kushuhudia uhaba wa maji kwa muda. Wazir wa maji Simon Chelugui anasema hali hii imechangiwa na ukosefu wa kiwango cha kutosha cha maji katika bwawa la Ndakaini.

Katika mkao na wanahabari,Chelgui amepuzilia mbali madai kuwa bwawa hilo limekosa uwezo wa kuhifadhi maji na kwamba mvua kubwa haijashuhudiwa katika maeneo ambako kuna mito ya kusambaza maji kwenye bwawa hilo.

Wakati huo huo Chelgui anasema kutokana mafuriko maeneo tofauti Garissa serikali tayari imeanza mikakati ya kuelekeza mafuriko hayo kwingine ili kuzuia maafa zaidi.

Show More

Related Articles