HabariMilele FmSwahili

Mvua kubwa inayonyesha nchini yaendelea kusababisha maafa

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini imeendelea kusababisha maafa, huko Garissa maeneo ya Bulapunda, Bula Estin na Mororo na Madogo huko Tanariver ni baadhi ya maeneo ambako tangu jana usiku viwango vya maji vimeendelea kuognezeka, wenyeji wakitaka muingilio wa serikali kuwanusuru. Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa anatarajiwa kuelekea huko Garissa leo kutathmini hali na kuongoza shughuli ya kutoa msaaa kwa waathiriwa. Huko Kilifi jeshi limeongoza oapresheni ya kuwaokoa wenyeji karibu 175 eneo la Garashi baada ya mto Sabaki kuvuta kingo zake. Hapa nairobi, uchukuzi umetatiza katika baadhi ya barabara wanaotumia magari wkaitakwia kuwa makini.

Show More

Related Articles