HabariSwahili

Wasiotambulika : Tunatambua Mkenya anayewahamasisha kuhusu madhara ya Zebaki

Mwezi uliopita, K24 ilipeperusha taarifa kuwahusu wachimba dhahabu kutoka kaunti ya Kakamega ikiangazia changamoto wanazozipitia ili  kupata dhahabu.
Kufuatia taarifa hiyo, jamaa mmoja aliona masaibu yao na athari za kiafya zinazowakumba haswa kina mama wajawazito wanaofanya kazi kwenye migodi, na kuamua kuanzisha mradi wa kuwaelimisha kuhusu athari za utumizi wa kemikali ya zebaki au mercury.
Joseph Chege, hutembelea migodi kote nchini akiwaelimisha kina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha kuepuka utumizi wa zebaki na kisha kuwapa njia mbadala za kutafuta dhahabu bila kutumia kemikali ya zebaki.

Show More

Related Articles