HabariMilele FmSwahili

Serikali yabuni jopo kazi la pamoja kuangazia mishahara ya wahadhiri

Serikali imebuni jopo kazi la pamoja ya maafisa kutoka wizara mbali mbali kuangazia mishara kwa wahadhiri wa vyuo vikuu. Kati ya mengine jopo hilo itafanya mashauriano kuhusu ofa mpya ya serikali kwa wahadhiri hao. Akizundua jopo hilo waziri wa elimu Amina Mohamed amewashauri wahadhiri kurejea kazini na kulipa jopo hilo fursa ya kutatua lalama zao. Jopo hilo litahitajika kuchunguza na kupendekeza mbinu za kukabili madai ya matumizi mabaya ya fedha na baadhi ya wahadhiri kukosa kufika madarasani kiholela. .

Show More

Related Articles