HabariMilele FmSwahili

Ruto: Hakuna haja ya taifa kushiriki kura ya maoni kufanyia mageuzi mfumo wa uongozi

Naibu rais William Ruto amesisitiza hakuna haja ya taifa kushiriki kura ya maoni kufanyia mageuzi mfumo wa uongozi. Akihutubia kongamano la magavana Kakamega, Ruto anasema taifa limetumia wakati mwingi kisiasa na itakua bora iwapo viongozi wataangazia kutimiza ahadi walizowapa wakenya wakati wa uchaguzi wa mwaka huu. Aidha,anasema baadhi ya masuala yanayoibuliwa kuhusu mfumo wa uongozi unaotumika kwa sasa yanaweza kutatuliwa bila kushiriki kura ya maoni.

Wakati uo huo, Ruto amewataka magavana kuwapa kazi ya kufanya manaibu wao akisema wengi wamesalia afisini bila majukumu na kupelekea kushiriki masuala yasiofaa.

Show More

Related Articles