HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Yaondia Ushuru Wa Tende.

Wito umetolewa kwa wfanyibiashara kutoongeza bei ya bidhaa ya tende haswa msimu huu ambapo jamii ya waislamu inatarajia kuingia katika mwezi mtukufu wa ramadhan.

Katibu mkuu wa baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK Sheikh Mohammed Khalifa amesema serikali imeondoa ushuru wa bidhaa hiyo hivyo inatakiwa iuzwe kwa bei ambayo kila muislamu ataweza kumudu kuinunua.

Khalifa aidha ameitaka idara ya usalama kuimarisha usalama kote nchini kabla na wakati wa mfungo wa ramadhani ili waumini waweze kufanya ibada zao bila usumbufu.

Huu ni mwaka wa tatu kwa serikali kuondoa ushuru wa tende wakati wa Ramadhan.

Show More

Related Articles