HabariMilele FmSwahili

Viongozi wammiminia sifa mwendazake Kennath Matiba

Mwendazake Kenneth Matiba amemiminiwa sifa tele na viongozi waliohudhuria misa ya wafu kwa ajili yake kaitika kanisa la All Saints Cathedral. Rais Uhuru Kenyatta amesema hakuna ambaye anaweza kulinganishwa na Matiba katika taifa hili. Amemtaja kama kiongozi aliyweka maslahi ya taifa mbele kushinda maslahi yake mwenye.
Akatumia fursa hiyo kuwapa changamoto viongozi kuiga mfano wake Matiba.
Naibu wake William Ruto pia akamtaja kama kiongozi aliyechangia pakubwa kwa demokrasi ambayo wakenya wanafurahia.

Show More

Related Articles