HabariPilipili FmPilipili FM News

Joho: Sina Tofauti Zozote Za Kibinafsi Na Serikali Ya Jubilee.

Gavana wa mombasa Hassan Ali Joho hatimaye amevunja kimya chake kuhusu ushirikiano wa Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa NASA Raila Odinga.

Akiongea mapema leo katika kaunti ya kakamega kunakofanyika kongamano la tano la ugatuzi, Joho ameshikilia kuwa hana pingamizi na maamuzi aliyochukua Odinga kushirikiana na rais Kenyatta.

Kuhusu msimamo wake dhidi ya serikali ya jubilee, gavana Joho ameshikilia kuwa hana tofauti zozote za kibinafsi na serikali ya jubilee, akisema kile ambacho wamekuwa wakipigania ni kuona wakenya wote wakihudumiwa kwa usawa.

 

 

Show More

Related Articles