HabariMilele FmSwahili

Kenya yaungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya Malaria

Kenya imeungana na ulimwengu katika maadhimisho ya siku ya Malaria ulimwenguni. Maadhimisho ya kitaifa yaandaliwa katika kaunti ya Kisii. Mkuu wa mpango wa kitaifa wa mapambano dhidi ya Malaria katika wizara ya afya Dr. Waqo Ejersa amezindua matembezi ya maadhimisho hayo. Maadhimisho ya mwaka huu yanayongozwa na kauli mbiu nimejitolea kupambana na Malaria changamoto ikitolewa kwa wakenya kutafuta matibabu upesi wanapohisi dalili za ugonjwa huo. Wizara ya afya imetoa hakikisho kuwa asilimia 98 ya vituo vya afya nchini vina uwezo wa kupima na kuwahudumia wagonjwa wa Malaria kikamilifu. Wizara hiyo pia imedokeza kuwa visa vya maambukizi ya Malaria vimepungua kutoka asilimia 11 hadi nane katika miaka mitano iliyopita.

Show More

Related Articles