HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Maseneta na magavana watofautiana kuhusu hazina ya wadi

Magavana wametofautiana pakubwa na msukumo wa bunge la senati, wa kutaka kupasisha mswada ambao iwapo utakuwa sheria, basi maeneo ya uwakilishi wadi yatapokea mgao wa fedha za kufanikisha maendeleo, ambao umekisiwa huenda utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 21.8.
Kwenye siku ya kwanza ya kongamano la ugatuzi, maseneta walikuwa wamegusia kuwa wataunga mkono mswada huo kwenye bunge la senate, na sasa magavana wanadai kuwa kutaibuka mtafaruku wa kisheria iwapo hilo litatimia.

Show More

Related Articles