HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Barabara ya Mai-Mahiu- Narok yafungwa kwa mara nyingine

Maelfu ya watu wamepoteza makao huku mamia wengine wakinusurika kifo kufuatia ongezeko la mafuriko maeneo tofauti nchini.
Mito kadha imevunja kingo zake huku barabara ya Mai Mahiu kuelekea Narok ikaharibiwa kwa mara nyingine tena baada ya maji ya mafuriko kufunika sehemu kubwa ya barabara kwa tope.
Rais Uhuru Kenyatta, ambaye hangeweza kuhudhuria kongamano la ugatuzi Kakamega kutokana na hali mbaya ya anga, kwa upande wake amewataka magavana kote nchini kutumia msimu huu wa mvua kuhakikisha maji ya mafuriko yanatekwa ili kutumiwa baadaye kwa ukulima.

Show More

Related Articles