HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Ugatuzi : Kenyatta amehimiza matumizi bora ya raslimali za umma

Rais Uhuru Kenyatta ametilia pondo umuhimu wa matumizi bora ya fedha zinazopaniwa kupiga jeki maendeleo katika kaunti kwenye lengo la kuboresha maisha ya wakenya.
Kenyatta ambaye amezindua mkopo wa shilingi bilioni hamsini kukadiria utendakazi kwenye kaunti amewaonya wale wote watakaohusika na ufisadi pamoja na kupokea mshahara bila kufanya kazi kwamba chuma chao ki motoni..
Kenyatta ambaye hakuelekea kaunti ya Kakamega kunako andaliwa kongamano la magavana kutokana na hali mbaya ya anga alihutubia kongamano kwa njia ya video ambapo amesisitiza haja ya magavana kusukuma ajenda nne kuu za serikali ya Jubilee.

Show More

Related Articles