HabariMilele FmSwahili

Rais atoa rambi rambi kwa jamaa za waliofariki kutokana mafuriko nchini

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi rambi kwa jamaa na marafiki kwa wakenya ambao wamefariki kutokana na mvua inayoendeelea kuponda nchini. Akitoa hotuba yake kwa kongamanao la ugatuzi linaloendelea Kakamega akiwa katika ikulu yake rais hapa Nairobi, Uhuru anasema hali mbaya ya hewa ndio imemzuia kufika kwenye kongamano hilo. Aidha amewataka wakenya kuwa waangalifu msimu huu kuhakikisha hawatembelei au kuishi maeneo ya chini na hatari kwa mafuriko. Wakati huo amewataka wakenya kuyavuna maji hayo ya mvua akisema yatasaidia taifa wakati wa ukame

Show More

Related Articles