HabariMilele FmSwahili

Murkomen atetea maseneta dhidi ya shtuma za kutatiza utendakazi wa magavana

Kiongozi wa wengi katika seneti Kipchumba Murkomen amewatetea maseneta dhidi ya shtuma wanatatiza utendakazi wa magavana. Akihutubu kwenye kongamano la tano la magavana huko Kakamega, Murkomena anasema katiba imeweka bayana majukumu baina ya maseneta na magavana hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anafanikisha majukumu hayo. Hata hivyo,amewaonya maseneta dhidi ya kutumia mialiko ya magavana kufika mbele yao kuwadhalilisha hadharani akisema hatua hiyoi itazisha uhasama baina yao.

Show More

Related Articles