HabariMilele FmSwahili

Kongamano la tano la ugatuzi laanza rasmi katika shule ya upili ya Kakamega

Kongamano la tano la ugatuzi limeanza rasmi katika shule ya upili ya Kakamega. Viongozi wakuu walioalikwa tayari wanatoa hotuba zao huku rais Uhuru Kenyatta akiratibiwa kufungua kongamano hilo rasmi muda mfupi kuanzia sasa. Kiongozi wa wachache katika bunge la seneti James Orengo ambaye tayari amehutubu anasema kuna haja ya kuongezwa mgao unaotengewa serikali za kaunti kufanikisha maendeleo mashinani.

Aidha, Orengo amesifia salamu za kihistoria baina ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga akisema mwafaka wao sasa unatoa nafasi ya viongozi wote kushirikiana.

Show More

Related Articles