HabariPilipili FmPilipili FM News

IEBC Yapewa Changamoto Kutatua Matatizo Yao.

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imeshauriwa kutathmini uwezo wake katika kuleta suluhu ya mizozo ya mipaka, ambayo imeonekana kuzikumba kaunti mbali mbali nchini, ikiwemo kaunti za kwale na Taita-taveta.

Hiyo ni kauli ya baraza la wazee kaunti ya Taita Taveta kupitia mwenyekiti Ronald Mwasi, ambaye amesema IEBC imekuwa ikitoa uamuzi wake kwa kuegemea maamuzi ya wanasiasa , jambo ambalo limechangia kutoafikiwa mwafaka ,hasa  ikizingatiwa kuwa wanasiasa hushindwa kutoa mwelekeo unaostahili.

Show More

Related Articles