HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Kuu Yahimizwa Kuongeza Pesa Kwa Kaunti.

Changamoto za kifedha, ufisadi pamoja na maendeleo ya ugatuzi katika kaunti mbalimbali nchini, zinatarajiwa kupewa kipao mbele, katika kongamano la magavana ambalo linafunguliwa rasmi leo na rais Uhuru Kenyatta.

Haya yamesemwa na gavana wa Kwale Salim Mvurya

Kwa upande wake seneta wa Siaya James Orengo ametoa changamoto kwa serikali ya kitaifa kuongeza mgao wa pesa za kaunti, sawia na kusawazisha ugavi wa mapato ya taifa ili kuhakikisha serikali za kaunti zinawezeshwa kutekeleza maendeleo.

Wakati huo huo Orengo amewataka magavana kutumia kongamano hilo kujadili kwa kina jinsi ya kujaza nafasi ya gavana na naibu wake ili kuepuka migogoro ya kisheria pale mmoja anapoaga dunia akitolea mfano kaunti ya Nyeri na Nairobi.

Show More

Related Articles