MichezoPilipili FmPilipili FM News

Wanamichezo Waonywa Dhidi Ya Miraa.

Wanamichezo wamehimizwa kutotumia dawa zilizoharamishwa michezoni ili kuepuka kufungiwa katika mashindano ya kitaifa na yakimataifa.

Akionge hapa mjini Mombasa mkuu mtendaji wa shirika la kupambana na dawa zilizoharamishwa michezoni ADAK Juphter Rugut amewadokezea wanamichezo kujiepusha kabisa na vitendo vya kusisimua misuli kinyume cha sheria.

Wakati huohuo mkuu huyo ameweka bayana kuwa miraa ni miongoni mwa bidhaa ambayo huchangia wanamichezo kupatikana na hatia ya kutoshiriki michezo ya kimataifa hivyo amewarai wakaazi wa Mombasa wanaohusika na michezo kuwahamasisha wachezaji kuhusiana na swala hilo.

Ameyasema hayo wakati wa warsha ya kuihamasisha timu ya Bandari kuhusiana na athari za kutumia dawa za kutitimua misuli.

Show More

Related Articles