HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Wenyeji Murang’a wawageuza tumbiri kuwa kitoweo kulipiza kisasi

Kero ya tumbiri katika kaunti ya Murang’a imekuwa ikiendelea kwa muda sasa.

Na kwa muda huo, wanyama hao ambao wana hulka sawa na binadamu, wameerevuka zaidi ya mitego wanayoekewa na serikali ya kaunti pamoja na shirika la huduma kwa wanyamapori, KWS ili kuwanasa.
Ghadhabu ya wakaazi haswa katika kaunti ndogo ya makuyu kutokana na uharibifu waliokadiria umepelekea wakaazi kuanza kuwafanya kitoweo tumbiri wanapowanasa.

Mwanahabari wetu Grace Kuria alikita kambi katika kaunti hiyo na kushuhudia hayo yote na sasa ametuandalia taarifa hiyo kwa ukamilifu kwenye makala kitoweo cha usumbufu.

Show More

Related Articles