HabariMilele FmSwahili

Watu 2 wanaodaiwa kumdhulumu mwangalizi wa uchaguzi mdogo wa Ruguru Nyeri wafikishwa mahakamani

Watu wawili wanaodaiwa kumdhulumu mwangalizi wa uchaguzi katika kituo cha Kiamariga wakati wa uchaghuzi mdogo wa Ruguru huko Nyeri wamefikishwa mahakamani huko Karatina na kushtakiwa. James Wanjohi na Jackson Ndegwa walifikishwa mbele ya hakimu mkuu Florence Macharia na kuachilwia kwa bondi ya shilingi 20000 pesa taslimu kila mmoja. Wanadai kumdhulumu Martha Miano na pia kutumia lugha chafu dhidi yake. Upande wa upinzani hata hivyo uliomba kuzuilwia kwao zaidi kwa dai huenda wakatatiza uchunguzi za kisa hicho. Wakati huo huo kesi iliyowasilishwa dhidi ya mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ambaye pia anatuhumiwa kumtusi Miano, iliondolewa mbele ya mahakama hiyo na kupelekewa kwa afisi ya mkuu wa mahstka kwa uchunguzi zaidi.

Show More

Related Articles