Mediamax Network Limited

Sportpesa yarejesha udhamini wake katika kandanda humu nchini

Hatimaye ligi kuu humu nchini KPL imepata mdhamini hii ni baada ya kampuni ya Sportpesa kurejea na kusaini mkataba wa miaka mitatu . Kampuni hiyo pia imerejesha udhamini wake na shirikisho la kandanda FKF , klabu ya Gor Mahia na ile ya AFC Leopards.

Huyu hapa ni mkurugenzi mkuu wa sportpesa Ronald Karauri akieleza undani wa makubaliano yao .Rais wa shirikisho la kandanda humu nchini FKF Nick Mwendwa ameishukuru Sportpesa kwa uamuzi wa kurejea katika shugli nzima ya kudhamini kandanda jambo analosema litapiga jeki sekta hiyo .Mapema mwaka huu kampuni ya sportpesa ilijiondoa katika kudhamini michezo mbalimbali baada ya serikali kupitisha mswada kampuni za kucheza kamara zitatozwa asilimia 35 ya ushuru