HabariMilele FmSwahili

Familia kadhaa zahamishwa makwao baada ya mto Nyando kuvunja kingo zake

Familia kadhaa zimehamishwa makwao baada ya mto Nyando kaunti ya Kisumu kuvunja kingo zake. Shirika la msalaba mwekundu linasema tukio hilo la asubuhi hii linatokana na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo. Kwengineko wenyeji eneo la Kibingei, kaunti ndogo ya Tinderet wanakadiria hasara kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyoharibu mimea na madarasa ya shule ya msingi ya Kibingei pia ikiharibiwa. Kisa hiki kinajiri siku moja baada ya gavana Stephen Sang kutangaza maporomoko ya ardhi kama janga la kaunti hiyo na kutoa mwito kwa serikali kuu kuingilia kati.

Show More

Related Articles