HabariPilipili FmPilipili FM News

Harusi Za Usiku Zapigwa Marufuku Mombasa

Idara ya polisi kaunti ya Mombasa imepiga marufuku sherehe zote za harusi nyakati za usiku.

Hii ni baada ya video ya yakutisha  kuenea katika mitandao ya kijamii ikionyesha vijana waliokuwa wamejihami na visu na mapanga wakitembea katika eneo la majengo wakati wa usiku.

Kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara anasema tayari vijana watatu miongoni mwao wamejisalimisha kwa polisi.

Wakati huo huo Ipara ametoa hakikisho la usalama kwa wakaazi na wageni wanaozuru  kaunti ya Mombasa.

Show More

Related Articles