HabariSwahili

Watu 11 wamefariki kwenye barabara ya Nairobi-Mombasa

Watu 11 hii leo wameaga dunia kufuatia ajali mbili tofauti za barabarani. tisa ambao ni majirani katika mtaa wa Githurai 44 waliangamia walipokuwa wanarejea nyumbani kutoka hafla ya kulipa posa eneo la Loitoktok.
Safari yao hata hivyo ilikatizwa pindi gari walimokuwa wakisafiri lilipoligonga lori moja lililokuwa limeegeshwa barabarani katika eneo la kwa Mumbi kwenye barabara kuu ya Mombasa -Nairobi.
Kama mwanahabari wetu Grace Kuria anavyotuarifu, watu wengine wawili waliofariki eneo la Mlolongo ni wafuasi wa timu ya Gor Mahia waliokuwa wakielekea katika uga wa Machakos kutizama mechi.

Show More

Related Articles