HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Ruto amekana uwezekano wa kugawana nyadhifa za serikali na upinzani

Naibu wa Rais William Ruto amefutilia mbali uwezekano wa mpango wa kugawana mamlaka kati ya serikali na viongozi wachache wa upinzani akisema kushirikiana na upinzani haimaanishi ugawanyaji wa mamlaka.

Akizungumza katika sherehe ya mazishi kaunti ya Nandi, Ruto amesema nguvu zote za serikali zinaelekezwa katika kutekeleza ajenda nne muhimu za Jubilee kwa wakenya na wala sio mbinu za kuwatafutia wapinzani mamlaka ndani ya serikali.

Show More

Related Articles