BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Ali Kiba Aoa Rasmi Msichana Wa Mombasa.

Yea nikweli mwanangu anaolewa na msanii Kiba na tumeridhia kuolewa kwake kwani Ali Kiba ni mwanamume mzuri na mimi na Gavana Joho ni marafiki tu kifamilia na twashukuru kwa harusi hii”.Amesema Asma.

Baada ya fununu na udaku kuhusu msanii mkali kutoka Bongo Ali Kiba kusemekana anaoa hatimaye ile ngoja ngoja imekwishwa kwani msanii huyo ameozeshwa rasmi msichana Amina Khelef Ahmed Salim kutoka Mombasa ambaye alianza kumchumbia mnamo mwaka 2016.

Nikkah hio imefanyika katika msikiti wa Ummul Kulthum Mosque na imeongozwa na Sheikh Mohammed Kagera

Na kulingana na wadaku wetu wa soga za usanii nikua zile ziara za msanii huyo kuja Mombasa kila mara na uhusiano wake wakaribu na gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho imetajwa pia sababu kuu yamsanii huyo kupata jiko lake upande wa pwani ya Kenya.

 

 

Akiongea katika kipindi cha MwakeMwake Live ndani ya Pilipili Fm na Gates Mgenge mamake Amina Asma Said amesema walimchunguza Ali Kiba na kujua ni mume mwema na wakaridhia kumuozesha mwana wao kwa hiari yao.

Pia Asma amesema yeye anaukuruba na gavana Joho kama rafiki wa familia yao na hawana uhusiano wa damu bali ni ule urafiki tu wa kifamilia.

“Yea nikweli mwanangu anaolewa na msanii Kiba na tumeridhia kuolewa kwake kwani Ali Kiba ni mwanamume mzuri na mimi na Gavana Joho ni marafiki tu kifamilia na twashukuru kwa harusi hii”.Amesema Asma.

Baada ya kutoka msikitini Ali Kiba amealikwa hafla ya chakula maarufu kama kombe la bwana harusi na kakake gavana Abubakar Joho eneo la Kizingo

Harusi hio imehudhuriwa na gavana wa kaunti ya Mombasa pamoja na wasanii wakutoka Mombasa wakiwemo Ali B,Dazlah,Chikuzee na Amour.

 

Hata hivyo waandishi wa habari walizuiliwa kuingia ndani kwani haki zote za kutangaza harusi hio mubashara zilinunuliwa na Azam Tv kutoka Tanzania.

Meza ya soga za usanii tunamtakiwa Ali Kiba na mkewe Amina maisha yenye heri na fanaka.

Show More

Related Articles