HabariMilele FmSwahili

Mahakama yaagiza kutiwa mbaroni mwenyekiti na maafisa wengine wa timu ya Gor Mahia kwa kukosa kufika kotini

Mahakama ya Nakuru imeagiza kutiwa mbaroni mwenyekiti wa  timu ya Gor Mahia  Ambrose Rachier na  viongozi wengine timu hiyo baada yao kukosa kufika Mahakamani. Hakimu Wilson Kitur alitoa agizo hilo  baada ya hoteli ya Donnies  huko Nakuru  kuishtaki timu hiyo kwa kukosa kulipa deni la shilingi nusu milioni. Mwenyekiti Rachier, John Pesa, Ronald Ingala na Jolani Obondo  wameshtakiwa baada yao kukosa kulipa pesa hizo ambazo zilitumiwa na timu  kwa mamkuli na pia  malazi 2015. Kulingana na hoteli hiyo ya Donnies timu hiyo ilitumia 524,730 kabla yao kufika katika uwanja wa afraha Nakuru katika michezo ya pre season game  kati yao na Western stima.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker