People Daily

Watalii Wanusurika Kifo Katika Eneo La Casorina Mjini Malindi

Zaidi ya watalii 15 wamenusurika kifo   baada ya hoteli mbili  kuchomeka maeneo ya Casorina mjini Malindi.

Kulingana na mumiliki wa Kenga Girama Resort Nicola Mosca  moto huo ulianzishwa na nyaya za umeme, kabla ya  kusambaa hadi katika hoteli jirani ya Dorado Cottages Resort.

Anasema moto huo umeteketeza mali ya mamilioni ya pesa katika hoteli zote mbili, ila hakuna mtu aliye jeruhiwa wakati wa mkasa huo.

Akithibitisha kisa hicho afisa mkuu wa polisi mjini malindi Matawa  Mchangi, amewaonya wananchi dhidi ya kupora mali za watalii katika mahoteli wakati wa mikasa kama hiyo, na  badala yake wasaidie kuokoa maisha ya watu pamoja na mali zao.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker