HabariMilele FmSwahili

Shirika la msalaba mwekundu kutumia millioni 20 kwa ujenzi wa miradi ya maji Lamu

Shirika la msalaba mwekundu litatumia shilingi milioni 20 kwa ujenzi wa miradi ya maji katika kaunti ya Lamu. Meneja wa Red cross sehemu hiyo anasema wanalenga kupungua matatizo wanayopitia wenyeji katika kusaka maji. Anasema tayari shilingi milioni 5 zimetumika kwenye ujenzi wa visima katika eneo ya Hindi. Kwenye mkao na gavana Fahim Twaha Hassan anasema wataweka mitambo ya kusafisha maji yanayotoka kwenye bahari ili yaweze kutumika nyumbani. Maeneo yanayolengwa ni Mbwajumwali,Kizingitin na Faza.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker