HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Makamishna 3 wamejiuzulu leo wakitia doa uongozi wa Chebukati

Makamishna watatu wa tume huru ya uchaguzi na kuratibu mipaka IEBC wamejiuzulu.

Naibu mwenyekiti Consolata Nkatha Maina, balozi Paul Kurgat na kamishna Margaret Mwachanya wanadai mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati ameshindwa kutoa mwelekeo kwenye utendakazi wa tume na badala yake ameigawanya tume kwa misingi ya matakwa ya kibinafsi yasiyo na msingi wa jukumu kuu la tume.
Wanastahili kuwasilisha barua za kujiuzulu kwao kwa rais Uhuru Kenyatta ili nafasi zao zitangazwe wazi na kuchapishwa kwenye gazetti rasmi la serikali kwa kipindi cha siku saba zijazo.

Kwa upande wake, Chebukati ameahidi kutoa mwelekeo kuhusu suala hilo hivi karibuni.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker