HabariMilele FmSwahili

Makamishena 3 wa IEBC wajiuzulu

Naibu mwenyekiti wa tume ya IEBC Connie Nkatha,makamishena profesa Paul Kurgat na Margret Mwachanya wamejiuzulu. Akitangaza kujiuzulu kwao,mwachanya anasema wameafikia uamuzi huo baada ya kukosa imani na mwenyekiti Wafula Chebukati. Mwachanya anasema Chebukati amekosa kutoa uongozi hitajika ndani ya IEBC hali iliosababisha malumbano ya mara kwa mara hasa baina yake na afisa mkuu Ezra Chiloba anayetumikia likizo ya lazima ya miezi mitatu.

Anasema kwa muda mrefu Chebukati amekua akitoa taarifa kudai ni msimamo wa tume ilihali ni msimamo wa kibinafsi hali iliowakera na kuamua kujiuzulu.

Kufuatia hatua hii,kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Kipchumba Murkomen amewapa matakaa ya siku 7 mwenyekiti Wafula Chebukati, makamishena Boya Molu na Abdi Guliye kujiuzulu mara moja lausivyo kubuniwe jopo la kuwachunguza.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker