HabariPilipili FmPilipili FM News

Makamishna Watatu Wa IEBC Wajiuzulu

Makamishna watatu wa tume ya uchaguzi nchini IEBC wamejiuzulu napema leo asubuhi.

Watatu hao ni Connie Maina, Mageret Mwachanya pamoja na Paul Kurgat.

Itakumbukwa kuwa watatu hao wamejiuzulu siku chache tu baada ya mgogoro mpya kuikumba tume hiyo.

Mwenyekiti wa tume hiyo wafula Chebukati amekuwa akimshinikiza afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Ezra Chiloba kuchukua likizo ya lazima, ili kupisha uchunguzi dhidi yake kufanywa, kuhusu tuhuma za ununuzi wa mali ya umma kinyume cha sheria.

Awali viongozi wa upinzani waliwataka makamishna wa tume hiyo kujiuzulu kwa kutokuwa na imani nao kusimamia chaguzi za mwaka jana.

Show More

Related Articles