HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanamke Aavya Mimba Na Kutupa Kijusi Katika Jaa taka, Taita.

Polisi mjini Voi kaunti ya Taita Taveta wameanzisha uchunguzi kutafuta mwanamke aliyeavya mimba, ya takribani miezi sita na kutupa kijusi  katika jaa la takaeneo la Sofia mjini humo.

Hili lilibainika baada ya watoto waliyokuwa wakicheza katika eneo hilo kuokota leso iliyotupwa, na   kuwaeleza wazazi wao waliofika kujionea masaibu hayo.

Akithibitisha kisa hicho kamanda  wa polisi mjini Voi Joseph Chesire amesema uchunguzi unaendeshwa na kwamba  watamnasa mshukiwa hivi karibuni

Show More

Related Articles