HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa Wa Ulaguzi Wa Mihadharati Kufikishwa Mahakamani Leo.

Washukiwa wanne wa ulanguzi wa dawa za kulevya wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya mombasa hii leo.

Wanne hao,  Said Rashid Musa mwenye umri wa miaka 32 na ambaye alikamatwa  katika eneo la majengo akiwa na vifuko sita vya dawa ya heroine, pamoja na Mahir sid Ahmed mwenye umri wa miaka 38 na ambaye alikamatwa eneo la bondeni, akiwa na madawa aina ya bugizi, bangi na heroine pamoja na vifaa vingine.

Mwengine ni Ramadhan Abdalla mwenye umri wa miaka 45 ambaye alikamatwa eneo la Ganjoni akiwa na dawa aina ya heroine, pamoja na Mohamed Feisal mwenye umri wa miaka 16, ambaye alikamatwa eneo la King’orani akiwa na misokoto mitatu ya bangi.

 

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker