HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Kero la ukimwi: Maambukizi ya virusi vya ukimwi kuongezeka

Japo kuwa viwango vya maambukizi  ya virusi vya ukimwi vimeripotiwa kuwa chini katika kaunti ya Tana River, ripoti kutoka  baraza la kudhibiti virusi vya ukimwi nchini (NACC) imesema kuwa huenda juhudi za kupambana na maambukizi kaunti hiyo  zikaathiriwa kutokana na viwango vya maambukizi mapya vinavyoshuhudiwa kaunti hiyo.

Walioathiriwa sasa  wanasemekana kuwa vijana kati ya umri wa miaka kumi na tano na ishirini na nne ambao pia wanasemekana kushiriki tendo la ndoa ovyoovyo bila kutumia kinga na kuzingatia usalama wao.
Unyanyapaa pia umesemekana kuchangia pakuu katika viwango vya juu vya maambukizi mapya kaunti hiyo.

Show More

Related Articles