MichezoMilele FmSwahili

Conselsus Kipruto ashinda dhahabu katika mbio za mita 3000 katika mashindano ya jumuia ya madola Australia

Conselsus Kipruto ameishindia Kenya medali ya dhahabu ya pili katika mashindano ya jumuia ya madola yanayoendelea mjini Gold Coast nchini Australia. Kipruto amewaongoza wenzake Abraham Kibiwot na Amos Kirui kunyakua dhahabu,shaba na fedha katika mbio za mita 3,000 zilizokamilika muda mfupi uliopita. Bingwa huyo wa dunia ameandikisha muda wa dakika nane,sekunde 10.08 kuipa Kenya dhahabu yake ya pili baada ya Wyckliff Kanyamal kushinda dhahabu ya kwanza jana katika mbio za mita 800.

Kufikia sasa Kenya ina medali 3 za shaba na nne za fedha. Aidha Kenya inatarajia kunyakua dhahabu ya 3 mwendo wa 1:45 mkenya Margret Nyairera atakapoingia ulingoni kupambana na Caster Semenya kutoka Afrika Kusini katika fainali za mita 800.

Show More

Related Articles