HabariMilele FmSwahili

Changamoto yatolewa kwa wanafunzi wa kike kuzingatia zaidi masomo ya Sayansi

Changamoto imetolewa kwa wanafunzi wa kike nchini kuzingatia zaidi masomo ya Sayansi. Kulingana na takwimu za shirika la umoja wa mataifa la elimu UNESCONI asilimia 9 pekee ya wanawake nchini waliofuzu na kusajiliwa kama wahandisi licha ya wanafunzi wengi wa kike nchini kuandikisha matokeo bora katika masomo ya sayansi Teknolojia na hesabati kwenye mitihani ya kitaifa. Katibu wa jinsia Zeinab Hussein anasema serikali imeweka mikakati ya kuwapa motisha wasichana kuchangamkia masomo hayo. Amesema hayo kwenye warsha iliyoandaliwa katika shule ya upili ya wasichana ya Machakos kutoa hamasishi kuhusu umuhimu wa masomo ya sanaysi.

Show More

Related Articles