HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wasiotambulika: Kituo cha kuosha magari ambacho wahudumu wana ulemavu wa ubongo

Kwenye makala ya wasiotambulika na hii leo tunamwangazia jamaa mmoja kutoka hapa jijini Nairobi ambaye ameamua kufungua kituo cha kuosha magari ampapo wafanyikazi wake wote ni watu wenye ulemavu wa ubongo almaarufu Autistic na Cerebral Palsy.
Maina Gatheru, mfanyikazi katika kampuni ya Kenya Power ana mtoto anayeugua ulemavu wa ubongo na alipoona mtoto wake amekomaa kuwa mtu mzima aliamua kumfungulia kituo hicho na kutafuta watu wengine wenye matatizo kama yake kama njia moja ya kuwapa mafunzo na mazoezi ya kufanya kazi ya kujiendeleza badala ya kutegemea familia zao.

Show More

Related Articles