HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Gavana Kahiga apendekeza Caroline Wanjiru Karugu kuwa Naibu wake , Nyeri

Gavana wa kaunti ya Nyeri Mutahi Kahiga amemteua Caroline Wanjiru Karugu kama naibu wake miezi sita baada ya kuwa afisini bila naibu gavana.

Kahiga amekuwa gavana wa kwanza kuafikia hilo baada ya mahakama ya upeo kutoa pendekezo la kutathmini katiba na kutoa ushauri kuhusiana na uteuzi wa naibu gavana huku bunge la seneti likiwa mbioni kubuni sheria itakayotumika kuafikia maamuzi kama hayo.

Bunge la kaunti ya Nyeri limetwikwa jukumu la kumpiga msasa Wanjiru Karugu baada ya spika wa bunge hilo kuwasilisha jina lake kama pendekezo la uteuzi wa gavana Kahiga.

Wanjiru Karugu ni msomi na pia kwa sasa amekuwa akihudumu kama mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Jabali Microserve.

Alifuzu na shahada ya kwanza kwenye somo la biashara kutoka chuo kikuu cha Daystar na pia amefuzu na stashahada kwenye somo la biashara kutoka chuo kikuu cha Frankfurt Ujerumani.

Show More

Related Articles