HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Gavana wa Benki Kuu atangaza viwango vya riba vya awali kurejelewa

Huenda ukatozwa riba ya juu uliyotozwa miaka miwili iliyopita iwapo una mkopo wa benki au unanuia kukopa iwapo bunge litakubali pendekezo la benki kuu nchini la kuondolewa kwa kiwango cha chini cha riba inayofaa kutozwa na benki.

Kwa sasa benki zimekuwa zikitoza riba isiyozidi asilimia 13.5 lakini iwapo kiwango hiki cha juu kitaondolewa,basi benki zitakuwa na uhuru wa kukutoza mimi na wewe riba ya hadi asilimia 25.

Je, mwelekeo utakuwa upi haswa ikizingatiwa Gavana wa Benki Kuu Patrick Njoroge amedokeza kuwa riba hiyo ya chini haifanyi kazi bali kuchangia katika kupunguza idadi ya wanaokopa ?

Show More

Related Articles