HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Rais mstaafu Moi akutana na Raila nyumbani kwake Kabarak

Kinara wa muungano wa upinzani Raila Odinga hii leo amefanya kikao na Rais Mstaafu Daniel Arap Moi katika makaazi yake eneo la Kabarak kaunti ya Baringo.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na msemaji wa Odinga Dennis Onyango, imesema Odinga alikwenda kumjulia hali mzee Moi na kumtakia afueni ya haraka haswa baada ya kipindi cha maradhi yaliyopelekea yeye kusafirishwa hadi nchini Israel.

Aidha Odinga na Moi wanasemekana kuzungumzia kwa mapana na marefu kuhusu jinsi atakavyomsaidia Rais Uhuru Kenyatta kutekeleza ajenda zake nne muhimu katika awamu yake ya pili ya uongozi.

Show More

Related Articles