HabariMilele FmSwahili

Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga apendekeza Caroline Karugu kama naibu wake

Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga, amempendekeza Caroline Wanjiru Karugu kama naibu wake. Karugu ni mwenyekiti wa kamati ya kiufundi katika kampuni ya uzalishaji kawi ya mvuke. Kwa sasa pia anahudumu kama murugenzi wa kampuni ya Jabali Microserve. Sasa anatarajiwa kupitia msasa wa bunge la kaunit hiyo kabla ya kuanza kuhudumu. Kahiga ambaye alichukau wadhfa wa ugavana Nyeri baad ya kifo chake Wahome Gakuru amekuwa bila naibu gavana kwa muda wa miezi minne iliypita.

Show More

Related Articles