HabariPilipili FmPilipili FM News

Jamaa Adai Kunyolewa Na Majini Usiku.

Jamaa mmoja kutoka eneo la Bombo, Kiembeni amewachwa kinywa wazi baada ya Kuamka na kupata kama amenyolewa bila idhini yake.

Jonathan Munga ambaye ni mwendeshaji boda boda anahoji kuwa alinyolewa miezi miwili iliyopita na majini   na kufikia sasa nywele hazijamea licha ya kutafuta suluhu hospitalini na Kanisani.

Licha ya kukiri  kuwepo nguvu za ushirikina katika zoezi hilo munga ameonekana akiwa na imani kwamba mola ata mkumbuka na nywele zake kumea tena

Show More

Related Articles