HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Wazazi walaumiwa kwa kutodhamini elimu ya vyuo vya kiufundi

Kufuatia tangazo la wizara ya elimu kutoa orodha ya wanafunzi waliofuzu kuingia vyuo vikuu tofauti nchini ,kizungumkuti kimejitokeza kufuatia idadi ndogo sana ya wanafunzi waliojitokeza kujiunga na vyuo vya kiufundi licha ya kupata alama za chini katika mtihani wa KCSE.
Kati ya wanafunzi zaidi ya elfu 200 waliopata alama ya d hadi E, ni wanafunzi elfu tano pekee waliotuma maombi wakitaka kujiunga na vyuo vya kiufundi ili kuendeleza masomo yao.
Wazazi wamelaumiwa kutokana na mwelekeo huu kwa kuwashinikiza watoto wao kupata alama za kuwawezesha kujiunga na vyuo vikuu na kukemea wanaopata alama za chini.

Show More

Related Articles