HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mume aliyetokwa na wadudu sehemu za siri Busia azidi kujuta

Taarifa tuliyoiangazia kuhusu jamaa kutoka kaunti ya Busia aliyekuwa akitokwa na wadudu katika sehemu zake nyeti baada ya kula uroda na mke wa mwajiri wake iliibua hisia kali , huku wengine wakisema kuwa haikuwa taarifa ya ukweli.
Tumelivalia njuga suala hilo tena , na kurejea nyumbani kwa mwathiriwa, ambaye mamake anakiri kuwa aliona mwanawe akitokwa na wadudu kutoka sehemu zake za siri , na vilevile kuongezea kuwa suala la uchawi sio geni katika eneo hilo.
Kama Frankline Macharia anavyosimulia , cha kushangaza ni kuwa licha ya kula uroda na mke wa mwajiri wake, muathirwa ana wake wengine wawili.

Show More

Related Articles