HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Shughuli zasimama kwa muda Kabarbet kufuatia kioja hicho

Kizaazaa kilitandaa katika mji wa Kabarnet, kaunti ya Baringo mapema hii leo baada ya bumba la nyuki kuamuwa kukita kambi juu ya pikipiki moja iliyokuwa imeegezwa pembezoni mwa jengo moja mashuhuri mjini humo.
Kinyume na walivotarajia aidha nyuki hao hawakuvamia mkaazi yeyote huku baadhi ya watu wakisema kwamba walikuwa ni baraka kutoka maulana, wengine wakida ushirikina.
Hii ni tukio la tatu kushuhudiwa mwaka huu kwani tukio sawia lilitendeka humo ambapo mhudumu wa bodaboda pamoja na wakaazi wa mji huo walivamiwa na nyuki hao.

Show More

Related Articles