HabariMilele FmSwahili

Serikali ya kaunti ya Nairobi yaanza kubomoa vibanda vilivyojengwa katika maeneo ya kuegesha magari hapa jijini

Serikali ya kaunti ya Nairobi imeanzisha ubomozi wa vibanda vilivyojengwa katika maeneo ya kuegesha magari hapa jijini. Maafisa wa kaunti kwa sasa wanaendesha ubomozi huo katika kituo cha Ngara kwa lengo la kutoa nafasi kwa magari. Mkurugenzi wa utendakazi kaunti ya Nairobi Peter Mbaya anasema wachuuzi katika vituo hivyo walipewa makataa ya majuma mawili kuondoka. Anasema lengo la kubomoa vibanda hivyo ni kufanikisha mpango wa kupunguza msongamano kati kati ya jiji.

Show More

Related Articles