HabariMilele FmSwahili

Serikali yaelezea imani ya kuimarika kwa uhusiano baina ya Kenya na sudan kiuchumi

Serikali imeelezea imani ya kuimarika kwa uhusiano baina ya Kenya na Sudan katika maswala ya kiuchumi. Naibu rais William Ruto aliye katika ziara ya siku tatu nchini Sudan amesema Kenya inanuia kuboresha utendakazi wa sekta mbali mbali kwa lengo la kuwanufaisha wananchi. Amehimiza pia ubadilishaji ujuzi na wataalamu kutoka nya nja mbali mbali katika mataifa yote mawili. ametaja nyanja za kilimo elimu na usalama kuwa baadhi ya ambazo nchi zote zinafaa kushirikiana kuboresha. Naibu rais amesema hayo katika mkao na waziri mkuu wa Sudan kusini Bakri Hassan Saleh jijini Khartoum .

Show More

Related Articles