HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Mvinyo wa Kitamaduni: Mkaazi wa Tharaka Nithi atengeneza kiwanda cha tembo asili

Je wajua kuwa kwa muda mrefu katika karne iliyopita chini ya utawala wa kikoloni wakenya hawakuruhusiwa kubugia tembo inayouzwa ikiwa kwenye chupa kwani ilikuwa ni haki ya mkoloni pekee yake?

Uongozi huo wa kikoloni pia uliwekea vikwazo utayarishaji wa mvinyo wa kitamaduni kama vile muratina, na busaa. Vileo hivyo vikikubalika tu nyakati za sherehe.

Sheria hizi zikapelekea utayarishaji na ubugiaji wa tembo mafichoni na hivyo kusababisha ukuaji wa uraibu wa vileo haramu kadri idadi ya watu ilivyozidi.

Na huku serikali ikijibidiisha kuangamiza uraibu huu wenye uwezo wa kuzua janga la kitaifa.

Mwanahabari wetu Zawadi Mudibo atusimulia kisa cha Mzee Albert Gitari kutoka Tharaka Nithi ambaye madhumuni yake ni kugema tembo mbadala kwa bei nafuu ili kuzuia maafa.

Show More

Related Articles