HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi 4 wa shule ya wavulana ya Jamhuri walioshtakiwa kufuatia vurugu shuleni humo waachiliwa

Wanafunzi wanne wa shule ya wavulana ya Jamhuri walioshtakiwa kufuatia vurugu zilizokua shule hiyo mapema mwaka huu wameachilwia huru. Wanne hao wameachiliwa baada ya walalamihsi wawili waliodaiwa kudhulumiwa na wanafunzi hao kuondoa kesi hiyo. Hakimu Francis Andayi hata hivyo amewapa onyo wanafunzi hao dhidi ya kuhusika kaitka vurugu.
Mawakili waakilishi kutoka pande zote wameelezea kuridhishwa na uamuzi huo wakiahidi kutekeleza agizo la hakimu Anday kuhakikisha maridhiano katika shule hiyo.
Wanafunzi hao walikamatwa kufuatia vurugu zinazodaiwa kuzuka baina ya wanafunzi kuhusiana na misimamo ya dini.

Show More

Related Articles